Kamisheini ya Ardhi imo katika matayarisho ya mfumo wa mradi unganishi wa usimamizi wa usajili wa ardhi ujulikanao LARIS ambao ni mfumo suluhisho la migogoro ya ardhi ambao unatarjiwa kuanzia mwaka 2025.
Akigusia mradi huo na utekelezaji wake kwa wajumbe wa bodi ya kamisheni ya ardhi Afisa Tehama kamishein ya ardhi Ibrahim Khalid Mambo amesema mfumo huo utarahisisha utendaji kazi kwa njia ya kidgital ambapo tayari kwa nchi nyingi za afrika wameshanza na wamefanikiwa na umekuwa na faida kubwa kwa wananchi.
Katibu mtendaji kamisheini ya ardhi Dr Abdul Nasir hikmany amesema matarajio ya mfumo huo ni kuiwezesha kamishein kufanya kazi zake kwa urahisi zaidi na pia mfumo huo utakuwa pia ni rahisi kwa wananchi katika kufanya maombi kwa njia za kimtandao.
Nae mwenyekiti wa bodi ya kamishein ya ardhi Dr idrissa musilih hijjja amesema mfumo utakapo anzana na kutekelezwa vyema utapunguza migogoro kwani mara nyingi migogoro ya ardhi inaibuliwa na wananchi hivyo bas kuja kwa mfumo huo kutaleta mabadiliko makubwa kwa jamii na kuitaka kamishein kuzidii kutoa elimu kwa wananchi zaidi .
Mafunzo hayo ya siku Moja kwa wajumbe wa bodi yameaandaliwa na kamishein ya ardhi (Cola) lengo ni kutoa uelewa kwa wajumbe kujua sheria za ardhi.
- Sunday 24 November 2024
- +255 774 108 011
- MAWASILIANO YETU