NYUMBANI > IDARA YA ARDHI
Tunajenga mfumo wa kisasa na rahisi wa kusajili ardhi nchini
Tunaweka kumbukumbu za haki ya matumizi ya ardhi
Tuwapatia wananchi uelewa wa kutosha kuhusiana na Usajili wa Ardhi
Idara ya Ardhi ni Idara inayohusika na utawala wa ardhi kwa ujumla. Idara hii inasimamia utekelezaji wa sheria tatu za ardhi. Sheria hizo ni Sheria ya Upatikanaji wa Haki ya Matumizi ya Ardhi Nambari 12 ya mwaka 1992, Sheria ya Kumtambua na Kumthibitisha Mwenye Haki ya Matumizi ya Ardhi Nambari 8 ya mwaka 1990 na Sheria ya Uthamini Nambari 5 ya mwaka 2015.
Majukumu ya Idara
- Kutayarisha Hati za umiliki wa haki ya matumizi ya Ardhi.
- Kutayarisha Vitambulisho vya umiliki wa matumizi ya Ardhi za Eka tatu
- Kutayarisha mikataba ya ukodishaji Ardhi
- Kuingiza taarifa za Ardhi katika mfumo wa kompyuta.
- Kukagua na kuhakiki maeneo ya kutayarishiwa mikataba ya ukodishaji wa ardhi.
- Kufanya ukaguzi katika maeneo ya uwekezaji.
- Kukagua na kuhakiki maeneo ya Eka tatu.
- Kufanya kazi za uthamini ardhi kwa madhumuni mbali mbali.
- Kufanya utambuzi wa ardhi katika maeneo mbali mbali.
Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi wa Ardhi na inazo na divisheni tano (5) kama ifuatavyo:
a. Divisheni ya Hati za Ardhi
Majukumu ya divisheni
- Ugawaji wa ardhi na utayarishaji Hati ya haki ya matumizi ya Ardhi.
- Usajili wa maombi ya ardhi/viwanja
- Kukusanya na Kuingiza taarifa za Ardhi katika mfumo wa kompyuta.
- Kuziweka taarifa za ardhi katika mpangilio mzuri kwa kurahishisha upatikanaji wake pale zinapohitajika.
- Kuandaa ripoti ya utekelezaji wa kazi za divisheni.
b. Divisheni ya Ukodishaji wa Ardhi
Majukumu ya divisheni
- Kutayarisha mikataba ya ukodishaji wa Ardhi
- Kukagua na kuhakiki maeneo ya kutayarishiwa mikataba ya ukodishaji wa ardhi.
- Kuingiza taarifa za Ardhi katika mfumo wa kompyuta.
- Kufanya ukaguzi wa maeneo ya uwekezaji.
- Kuziweka taarifa za ardhi katika mpangilio mzuri kwa kurahishisha upatikanaji wake pale zinapohitajika.
- Kuandaa ripoti ya utekelezaji wa kazi za divisheni.
c. Divisheni ya Eka
Majukumu ya divisheni
- Kutayarisha Vitambulisho vya matumizi ya Ardhi za Eka tatu.
- Kuingiza taarifa za Ardhi za mashamba katika mfumo wa kompyuta.
- Kukagua na kuhakiki maeneo ya Eka tatu.
- Kusuluhisha migogoro ya ardhi za mashamba ya eka.
- Kuziweka taarifa za ardhi katika mpangilio mzuri kwa kurahishisha upatikanaji wake pale zinapohitajika.
- Kuandaa ripoti ya utekelezaji wa kazi za divisheni.
d. Divisheni ya Uthamini wa Ardhi
Majukumu ya divisheni
- Kukusanya taarifa na maombi ya uthamini.
- Kukagua na kuhakiki maeneo ya kutiliwa thamani.
- Kufanya kazi za uthamini ardhi kwa madhumuni mbali mbali.
- Kuandaa ripoti na kuweka kumbukumbu za kazi za uthamini.
- Kufanya uthamini wa mali zinazohamishika na zisizohamishika kwa malengo mbali mbali.
- Kuandaa ripoti ya utekelezaji wa kazi za divisheni.
e. Divisheni ya Utambuzi wa Ardhi
Majukumu ya divisheni
- Kukusanya na Kuingiza taarifa za Ardhi katika mfumo wa kompyuta.
- Kutayarisha Hati za umiliki wa haki ya matumizi ya Ardhi.
- Kukagua na kuhakiki maeneo ya utambuzi
- Uwekaji kumbukumbu wa umiliki na uhaulishaji.
- Kuandaa ripoti ya utekelezaji wa kazi za divisheni.
Dira na Dhamira
Dira Yetu
Dira ya Wizara ni kuhakikisha kwamba Wananchi wote wa Zanzibar wanafaidika na huduma bora za Makaazi na matumizi mazuri ya Ardhi iliopo ili kukuza uchumi wa Nchini.
Dhamira Yetu
Wizara imejizatiti kutoa huduma zinazopatikana kwa uhakika , rahisi na endelevu kwa wananchi wote Pamoja na kuzingatia makaazi yaliyo nafuu na matumizi ya ardhi kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.