NYUMBANI > IDARA YA MIPANGO MIJI NA VIJIJI

Tunajenga mfumo wa kisasa na rahisi wa kusajili ardhi nchini

Tunaweka kumbukumbu za haki ya matumizi ya ardhi

Tuwapatia wananchi uelewa wa kutosha kuhusiana na Usajili wa Ardhi

Idara ya Mipango Miji na Vijiji inahusika na upangaji wa Miji na Vijiji. Idara hii inasimamia utekelezaji wa Sheria ya Mipango Miji na Vijiji (Decree Cap 85) ya mwaka 1955.

Majukumu ya Idara

  1. Kupanga matumizi bora na endelevu ya miji Zanzibar,
  2. Kusimamia maendeleo ya ardhi katika Miji, Mikoani na maeneo ya fukwe n.k.
  3. Kuimarisha Miji ili kukuza uchumi na kuleta Maisha bora
  4. Kupanga na kusimamia maendeleo ya makaazi nchini kwa mujibu wa sheria na sera za maendeleo.
  5. Kuwa mwelekezaji na mshauri mkuu wa Serikali katika mipango ya maendeleo ya ardhi
  6. Kufanya tafiti mbali mbali zinazohusiana na mipango miji.
  7. Kusaidiana na Manispaa, Mabaraza ya Miiji na Halmashauri za Wilaya ili kudhibiti ujenzi holela.
  8. Kutayarisha Mipango ya Matumizi ya Ardhi katika Miji na Vijiji na kusimamia utekelezaji wake.
  9. Kutayarisha mipango ya maendeleo ya miji na viwango vya uendelezaji wa miji na vijiji (planning guide lines)
  10. Kuyapanga na kuyaendeleza maeneo ambayo yamejengwa kiholela (improvement plans)
  11. Kushauri na kufanya mapitio na marekebisho ya kanuni na sheria zinazohusiana na mipango miji.
  12. Kutoa elimu kwa jamii katika masuala ya Matumizi Bora ya Ardhi na Maendeleo ya Miji na Vijiji na kuwashirikisha wadau katika hatua za mwanzo za kutayarisha mipango hiyo ili iwe endelevu na kukubalika.

Idara hii inasimamiwa na Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji na inazo divisheni tatu (3) ambazo ni:

a.   Divisheni ya Mipango ya Uendelezaji wa Miji na Maeneo ya Wazi

Majukumu ya divisheni

  1. Kupanga matumizi bora na endelevu ya miji ya Zanzibar;
  2. Kusimamia maendeleo ya ardhi katika Miji na maeneo ya fukwe.
  3. Kuimarisha Miji ili kukuza uchumi na kuleta Maisha bora;
  4. Kupanga na kusimamia maendeleo ya makaazi nchini kwa mujibu wa Sheria na Sera za maendeleo na kuwa mwelekezaji na mshauri mkuu wa Serikali katika kuandaa mipango ya maendeleo ya ardhi.
  5. Ukaguzi wa maeneo yaliyopangwa na kutolewa miongozo;
  6. Kusanifu maeneo ya wazi.
  7. Kuandaa ripoti ya utekelezaji wa kazi za divisheni.

b.   Divisheni ya Mipango ya Uendelezaji katika maeneo ya Nje ya Miji (Mikoani)

Majukumu ya divisheni

  1. Kutayarisha Mipango ya Matumizi ya Ardhi katika Vijiji na kusimamia utekelezaji wake;
  2. Kudhibiti ujenzi holela kwa kushirikiana na Manispaa, Mabaraza ya Miji na Halmashauri za Wilaya.
  3. Kukagua maeneo yaliyopangwa na kutolewa miongozo;
  4. Kutayarisha mipango ya maendeleo na viwango vya uendelezaji wa vijiji (planning guide lines).
  5. Kuyapanga na kuyaendeleza maeneo ambayo yamejengwa kiholela (improvement plans).
  6. Kuandaa ripoti ya utekelezaji wa kazi za divisheni.

c.   Divisheni ya Utafiti na Kumbukumbu

Majukumu ya divisheni

  1. Kufanya tafiti mbali mbali zinazohusiana na mipango miji.
  2. Kutayarisha mipango ya utafiti wa kimaendeleo kwa kuzingatia viwango vya uendelezaji wa miji na vijiji (planning guide lines);
  3. Kusimamia na kutunza kumbukumbu zote zinazihusu mipango ya miji na vijiji.
  4. Kufanya mapitio na marekebisho ya kanuni na sheria zinazohusiana na mipango miji.
  5. Kutoa elimu kwa jamii katika masuala ya mipango na Matumizi Bora ya Ardhi na Maendeleo ya Miji na Vijiji na kuwashirikisha wadau katika hatua za mwanzo za kutayarisha mipango hiyo ili iwe endelevu na kukubalika.

Kuandaa ripoti ya utekelezaji wa kazi za divisheni

Dira na Dhamira

Dira Yetu

Dira ya Wizara ni kuhakikisha kwamba Wananchi wote wa Zanzibar wanafaidika na huduma bora za Makaazi na matumizi mazuri ya Ardhi iliopo ili kukuza uchumi wa Nchini.

Dhamira Yetu

Wizara imejizatiti kutoa huduma zinazopatikana kwa uhakika , rahisi na endelevu kwa wananchi wote Pamoja na kuzingatia makaazi yaliyo nafuu na matumizi ya ardhi kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.