Kamisheini ya Ardhi imo katika matayarisho  ya mfumo   wa mradi unganishi  wa usimamizi wa usajili wa ardhi  ujulikanao LARIS ambao  ni mfumo  suluhisho la migogoro ya ardhi ambao  unatarjiwa kuanzia mwaka 2025.
Akigusia mradi huo na utekelezaji wake kwa wajumbe wa bodi ya kamisheni ya ardhi Afisa Tehama  kamishein  ya ardhi    Ibrahim  Khalid Mambo amesema  mfumo huo  utarahisisha utendaji kazi kwa njia ya kidgital ambapo tayari kwa nchi  nyingi za afrika   wameshanza na wamefanikiwa na umekuwa na faida kubwa kwa wananchi.
Katibu mtendaji kamisheini ya ardhi   Dr  Abdul Nasir hikmany amesema matarajio ya mfumo huo  ni kuiwezesha kamishein   kufanya kazi zake kwa urahisi  zaidi  na pia  mfumo huo utakuwa pia  ni rahisi kwa wananchi katika kufanya maombi kwa njia za kimtandao. 
Nae mwenyekiti wa bodi ya kamishein ya ardhi  Dr idrissa musilih hijjja amesema    mfumo utakapo anzana na kutekelezwa vyema utapunguza migogoro kwani mara nyingi migogoro ya ardhi  inaibuliwa na wananchi  hivyo bas kuja kwa mfumo huo kutaleta mabadiliko makubwa kwa jamii na kuitaka kamishein  kuzidii kutoa elimu kwa wananchi zaidi .
Mafunzo hayo ya siku Moja kwa wajumbe wa bodi yameaandaliwa na kamishein ya ardhi (Cola) lengo ni kutoa uelewa kwa wajumbe kujua sheria za ardhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *