NYUMBANI > AFISI YA MRAJIS WA ARDHI
Tunajenga mfumo wa kisasa na rahisi wa kusajili ardhi nchini
Tunaweka kumbukumbu za haki ya matumizi ya ardhi
Tuwapatia wananchi uelewa wa kutosha kuhusiana na Usajili wa Ardhi
Afisi ya Mrajis wa Ardhi ni Taasisi iliyoanzishwa kwa lengo la kusajili ardhi ya Zanzibar. Taasisi hii inasimamia Sheria ya Usajili wa Ardhi Nambari 10 ya mwaka 1990.
Afisi Mrajis wa Ardhi
Afisi hii imeundwa kutokana na kifungu nambari 6 (2) (d) cha sheria ya Kamisheni ya Ardhi nambari 6 ya mwaka 2015.
- Kufanya usajili wa ardhi kwa wale wenye hati ya haki ya matumizi ya ardhi.
- Kufanya uhakiki wa hati za haki ya matumizi ya ardhi kwa ajili ya usajili.
- Kuweka kumbukumbu za usajili wa ardhi katika Rejista la Usajili wa Ardhi.
- Kuyaendeleza kiusajili (subsequent registration) baadhi ya maeneo pale inapohitajika.
- Kuwapatia wananchi uelewa wa kutosha kuhusiana na Usajili wa Ardhi.
- Kuweka taarifa za miamala mbalimbali zinazohusiana na Regista la Ardhi kwa wakati.
- Kuweka kumbukumbu za haki ya matumizi ya ardhi kwa watu waliosajiliwa.
- Kujenga mfumo wa kisasa na rahisi wa kusajili ardhi nchini, utaoshirikisha wadau.
Afisi hii inaongozwa na Mrajis wa Ardhi akisaidiwa na Naibu Mrajis kwa ofisi ya Pemba na Wasaidizi wa Mrajis ambao wapo Unguja. Vile vile inazo divisheni tatu kwa kusimamia kazi za Usajili wa Ardhi kama zifuatazo:
a. Divisheni ya Usajili wa Ardhi
Majukumu ya divisheni
- Kufanya usajili wa ardhi kwa wale wenye hati ya haki ya matumizi ya ardhi.
- Kufanya uhakiki wa hati za haki ya matumizi ya ardhi kwa ajili ya usajili.
- Kutoa kadi za usajili wa ardhi
- Kusajili maeneo ya mirathi
- Kuandaa ripoti ya utekelezaji wa kazi za divisheni.
b. Divisheni ya Kuendeleza Usajili wa Ardhi
Majukumu ya divisheni
- Kusimamia na kuendeleza usajili wa ardhi.
- Kufanya uhakiki kwa maeneo yaliyosajiliwa.
- Kusimamia masuala ya utoaji wa elimu juu usajili wa ardhi.
- Kuandaa ripoti ya utekelezaji wa kazi za divisheni.
c. Divisheni ya Nyaraka na Kumbukumbu za Usajili wa Ardhi
Majukumu ya divisheni
- Kuweka kumbukumbu za usajili wa ardhi katika Rejista la Usajili wa Ardhi;
- Kuweka taarifa za miamala mbalimbali zinazohusiana na Regista la Ardhi kwa wakati.
- Kuweka kumbukumbu za haki ya matumizi ya ardhi kwa watu waliosajiliwa;
- Kujenga mfumo wa kisasa na rahisi wa kusajili ardhi nchini, utaoshirikisha wadau.
- Kuandaa ripoti ya utekelezaji wa kazi za divisheni.
Dira na Dhamira
Dira Yetu
Dira ya Wizara ni kuhakikisha kwamba Wananchi wote wa Zanzibar wanafaidika na huduma bora za Makaazi na matumizi mazuri ya Ardhi iliopo ili kukuza uchumi wa Nchini.
Dhamira Yetu
Wizara imejizatiti kutoa huduma zinazopatikana kwa uhakika , rahisi na endelevu kwa wananchi wote Pamoja na kuzingatia makaazi yaliyo nafuu na matumizi ya ardhi kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.