Tunajenga mfumo wa kisasa na rahisi wa kusajili ardhi nchini
Tunaweka kumbukumbu za haki ya matumizi ya ardhi
Tuwapatia wananchi uelewa wa kutosha kuhusiana na Usajili wa Ardhi
Divisheni za Idara Ardhi
- Divisheni ya Usajili wa Ardhi
- Divisheni ya Kuendeleza Usajili wa Ardhi
- Divisheni ya Nyaraka na Kumbukumbu za Usajili wa Ardhi
KUHUSU SISI
Kamisheni ya Ardhi ni chombo cha Serikali kilichoanzishwa kupitia Sheria Namba 6 ya mwaka 2015.
Lengo la kuanzishwa Kamisheni ya Ardhi ni kusimamia maswala ya ardhi katika kujenga uimara wa uongozi na rasilimali ya ardhi kwa ajili ya matumizi bora na maendeleo ya Taifa.
Ili kutimiza azma hiyo imeonekana ni vyema kuanzishwa chombo ambacho kitakuwa na uwezo wa kusimamia mambo yanayohusu ardhi kwa ujumla wake.
Ingawa kuna vyombo mbalimbali nchini ambavyo kwa njia moja au nyengine zinahusika na masuala ya ardhi, kwa kuanzishwa Kamisheni ya Ardhi mwaka 2015 mamlaka yote yanayohusika na usimamizi na utawala wa ardhi yamewekwa chini ya chombo kimoja ambacho ni Kamisheni ya Ardhi.
Hivyo, Wananchi wote wanatakiwa kutumia ardhi kwa mujibu wa maelekezo yanayotolewa na Kamisheni ya Ardhi na kutoa mashirikiano yao ili kuleta matumizi endelevu ya ardhi nchini.
Idara ya Upimaji na Ramani
Idara hii imeundwa kutokana na kifungu nambari 6(2)(b) cha sheria ya Kamisheni ya Ardhi nambari 6 ya mwaka 2015.
Wasiliana nasi juu ya mwongozo wa maswala ya ardhi!
info@kamisheniardhi.go.tz
+255 712 345 678
BODI YA
KAMISHENI YA ARDHI