NYUMBANI > IDARA YA UPIMAJI NA RAMANI

Tunajenga mfumo wa kisasa na rahisi wa kusajili ardhi nchini

Tunaweka kumbukumbu za haki ya matumizi ya ardhi

Tuwapatia wananchi uelewa wa kutosha kuhusiana na Usajili wa Ardhi

Majukumu ya Idara

  1. Kupima viwanja kwa matumizi mbalimbali
  2. Kupima vianzio vya Upimaji (Survey Control Points)
  3. Kusimamia kazi za kiuhandisi na upimaji wa baharini
  4. Kutoa na kuchapisha nakala za ramani
  5. Kutunza kumbukumbu za kazi zote za Upimaji na Ramani
  6. Kuhifadhi kumbukumbu za Ardhi nchini, kuwa katika Mfumo wa Taarifa za Ardhi nchini-Zanzíbar.
  7. Kutayarisha Ramani Msingi (Basemap) zinazoweza kutumika katika shughuli mbali mbali,
  8. Kuimarisha Upimaji wa mtandao wa alama za msingi ardhini na baharini (Control Points, Hydrography) kwa ajili ya utayarishaji ramani/chati za matumizi mbalimbali.
  9. Uwekaji wa mipaka ya kiutawala kwa kushirikiana na Afisi za Tawala za Mikoa kila inapohitajika
  10. Kusimamia Taaluma na maadili ya kazi za Upimaji na Ramani.
  11. Kujenga na kuimarisha Vituo vya Upimaji “Continuous Operating Reference Stations” (CORS).
  12. Kuimarisha kituo cha kupima kupwa na kujaa maji ya bahari “Tide gauge” kwa matumizi mbalimbali.
  13. Kuelimisha jamii juu ya Upimaji wa Ramani na umuhimu wa kumbukumbu zake.
  14. Kusimamia Taaluma na maadili ya kazi Upimaji na Ramani.
  15. Kushauri na kuandaa mapendekezo ya Sheria na Kanuni za Upimaji na Ramani kutokana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia duniani.

Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani na inazo divisheni tatu (3) ambazo ni:

a.     Divisheni ya Upimaji

Majukumu ya divisheni

  1. Kupima viwanja kwa matumizi mbalimbali
  1. Kuandaa mapendekezo ya Sheria na Kanuni za Upimaji
  2. Uwekaji wa mipaka ya kiutawala kwa kushirikiana na Afisi za Tawala za Mikoa.
  3. Kupima vianzio vya Upimaji (Survey Control Points).
  4. Kusimamia kazi za kihandisi na upimaji wa baharini.
  5. Kuimarisha Upimaji wa mtandao wa alama za msingi ardhini na baharini (Control Points, Hydrography) kwa ajili aya utayarishaji ramani/chati za matumizi mbalimbali.
  6. Kuanzisha Vituo vya Upimaji “Continuous Operating Reference Stations” (CORS).
  7. Kuimarisha kituo cha kupima kupwa na kujaa maji ya bahari “Tide gauge”
  8. Kuandaa ripoti ya utekelezaji wa kazi za divisheni.

b.     Divisheni ya ramani

Majukumu ya divisheni

  1. Kutoa na kuchapisha nakala za ramani.
  2. Kutayarisha Ramani Msingi (Basemap) zinazoweza kutumika katika shughuli mbali mbali.
  3. Kuimarisha na kuvirejesha vianzio vya Upimaji (Survey Control Points).
  4. Kuandaa mapendekezo ya Sheria na Kanuni za ramani
  5. Kuandaa ripoti ya utekelezaji wa kazi za divisheni.

.     Divisheni ya Kumbukumbu za Upimaji na Ramani

Majukumu ya divisheni

  1. Kutunza kumbukumbu za kazi zote za Upimaji na Ramani
  2. Kuratibu kumbukumbu za Ardhi nchini, kuwa katika Mfumo wa Taarifa za Ardhi nchini – Zanzíbar.
  3. Kuelimisha jamii juu ya Upimaji wa Ramani na umuhimu wa kumbukumbu zake.
  4. Kuandaa mapendekezo ya Sheria na Kanuni za Upimaji na Ramani.

Kuandaa ripoti ya utekelezaji wa kazi za divisheni

Dira na Dhamira

Dira Yetu

Dira ya Wizara ni kuhakikisha kwamba Wananchi wote wa Zanzibar wanafaidika na huduma bora za Makaazi na matumizi mazuri ya Ardhi iliopo ili kukuza uchumi wa Nchini.

Dhamira Yetu

Wizara imejizatiti kutoa huduma zinazopatikana kwa uhakika , rahisi na endelevu kwa wananchi wote Pamoja na kuzingatia makaazi yaliyo nafuu na matumizi ya ardhi kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.