NYUMBANI > KUHUSU SISI

Tunajenga mfumo wa kisasa na rahisi wa kusajili ardhi nchini

Tunaweka kumbukumbu za haki ya matumizi ya ardhi

Tuwapatia wananchi uelewa wa kutosha kuhusiana na Usajili wa Ardhi

KUHUSU SISI

Kamisheni ya Ardhi ni chombo cha Serikali kilichoanzishwa kupitia Sheria Namba 6 ya mwaka 2015.
Lengo la kuanzishwa Kamisheni ya Ardhi ni kusimamia maswala ya ardhi katika kujenga uimara wa uongozi na rasilimali ya ardhi kwa ajili ya matumizi bora na maendeleo ya Taifa.
Ili kutimiza azma hiyo imeonekana ni vyema kuanzishwa chombo ambacho kitakuwa na uwezo wa kusimamia mambo yanayohusu ardhi kwa ujumla wake.

UTAWALA KAMISHENI YA ARDHI

Muundo unaopendekezwa unaonesha uwepo wa Katibu Mtendaji, Idara tano (5) (ikiwemo Afisi ya Mrajis wa Ardhi), Afisi ya Uratibu – Pemba na Vitengo sita (6) vinavyojitegemea. Maelezo kuhusu muundo huu ni kama ifuatavyo:-

Sababu za kuanzishwa Kamisheni ya Ardhi

Kuna sababu kadhaa zilizopelekea kuanzishwa Kamisheni ya Ardhi miongoni mwa sababu hizo ni hizi zifuatazo:-

Kamisheni ya Ardhi imeundwa ili iwe chombo kinachounganisha Idara zote za ardhi katika mwamvuli na chini ya uongozi mmoja.
Hapo awali kabla ya kuanzishwa chombo hiki utawala wa ardhi na usimamizi ulikuwa umegawika kiidara ambapo kila Idara ilikuwa inafanya kazi zake wenyewe bila ya kuwepo chomboambacho kinaunganisha Idara zote za ardhi.

Kuwa na taasisi tofauti ambazo zinasimamia masuala ya ardhikulipelekea kuweko na urasimu katika utolewaji wa huduma katika sekta ya ardhi.
Hivyo Serikali iliamua kuunda taasisi ambayo itaziunganisha Taasisi zote za ardhi na hivyo kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.

Kutokuwepo kwa chombo kimoja kinachosimamia utekelezaji wa Sheria na Sera ya Ardhi kulipelekea kurejesha nyuma usimamizi na utekelezaji wa Sheria za Ardhi. Hivyo Kamisheni ya Ardhi iliundwa ili iwe na Mamlaka kamili ya kusimamia sheria zoteza Ardhi pamoja na Sera ya Ardhi.

Dira na Dhamira

Dira Yetu

Dira ya Wizara ni kuhakikisha kwamba Wananchi wote wa Zanzibar wanafaidika na huduma bora za Makaazi na matumizi mazuri ya Ardhi iliopo ili kukuza uchumi wa Nchini.

Dhamira Yetu

Wizara imejizatiti kutoa huduma zinazopatikana kwa uhakika , rahisi na endelevu kwa wananchi wote Pamoja na kuzingatia makaazi yaliyo nafuu na matumizi ya ardhi kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

BODI YA

KAMISHENI YA ARDHI

MUUNDO MPYA WA

KAMISHENI YA ARDHI